Mlipuko umetokea kwenye kituo cha subway cha Parsons Green kilichoko magharibi mwa mji wa London Uingereza leo asubuhi.
Mashuhuda wanasema mlipuko huo umesababisha baadhi ya watu kuungua, huku idadi kubwa ya majeruhi ikisababishwa na wingi wa watu waliokuwa wakikimbia kutoka eneo hilo.
Mlipuko huo ulisababisha vurugu katika eneo hilo kutokana na huduma za subway kufungwa na polisi kuzuia watu kukaribia eneo la tukio.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |