• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Gambia aweka jiwe la msingi la kituo cha mikutano kinachojengwa na kampuni ya China

    (GMT+08:00) 2017-09-15 19:04:04

    Rais Adam Barrow wa Gambia ameweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano kinachojengwa kwa ufadhili wa China.

    Rais Barrow amesema urafiki na ushirikiano kati ya Gambia na China unaimarika ndani ya mfumo wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kwamba uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili unajengwa kwenye msingi wa kuheshimiana na maslahi ya pamoja.

    Balozi wa China nchini Gambia Zhang Jiming amesema, kituo hicho ni mradi wa kwanza mkubwa wa ushirikiano kati ya China na Gambia tangu nchi hizo zirejeshe uhusiano wa kibalozi. Pia amesema, mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 50 ni mkubwa zaidi katika uhusiano wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako