• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Mashariki wasema mashambulizi ya kigaidi yameongezeka nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-16 18:26:17
    Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Mashariki IGAD siku ya ijumaa imesema imesikitishwa na mashambulizi ya kigaidi hivi karibuni nchini Somalia yaliyofanywa na kundi la kiislamu la Al-Shabaab, na kuwaua watu kadhaa na wengine kujeruhiwa.

    Nchi wanachama wa IGAD zimesema, Al-Shabaab inajaribu kuharibu faida ambazo watu na serikali ya Somalia wamepata kithabiti, kufanya kazi kwa bidii na matumaini.

    Nchi wanachama wa IGAD zimeridhishwa na ujasiri unaofanywa na askari wa serikali ya somalia katika kulinda nchi yao, serikali yao na watu wao dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara.

    wapiganaji wa Al-Shabaab hivi karibuni wameongeza mashambulizi dhidi ya vikosi vya Umoja wa Afrika na majeshi ya Somalia huko Mogadishu na kusini mwa Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako