• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yaimarisha kiwango cha ulinzi dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-09-16 18:26:40

    Waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May amesema serikali imeimarisha ulinzi na kueleza kuwa kuna uwezekano wa mashambulizi zaidi ya kigaidi hivi karibuni nchini humo.

    Bi. May amesema serikali yake imeamua kuimarisha ulinzi baada ya mlipuko uliotokea katika kituo cha treni za chini cha Parson Green Ijumaa asubuhi huko London.

    polisi wamesema mlipuko huo ni shambulizi la kigaidi, na wanaendelea na upelelezi kumtambua mtu anayehusika na mlipuko huo kwa kuweka bomu la kutengenezwa nyumbani kwenye treni.

    Mlipuko huo umesababisha zaidi ya watu 29 kujeruhiwa, wengi wao wakitibiwa hospitali kutokana na majeraha ya kuungua kwa moto.

    Kundi la kigaidi la IS siku ya ijumaa usiku lilidai kuhusika na mashambulizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako