• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yarekebisha utabiri wa ukuaji wa uchumi kuwa asilimia 5.5 kwa mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2017-09-16 18:56:28

    Kenya imerekebisha utabiri wa ukuaji wa uchumi wa mwaka 2017 kuwa asilimia 5.5 kutokana mvutano katika uchaguzi mkuu.

    Waziri wa fedha bwana Henry Rotich aliwaambia waandishi wa habari huko Nairobi kuwa serikali inasubiri takwimu za ukuaji kwa robo ya pili ya mwaka 2017 ili kufanya utabiri sahihi wa jumla ya ukuaji wa jumla wa bidhaa za ndani kwa mwaka 2017.

    Rotich amesema kurefushwa kwa kipindi cha uchaguzi mkuu kutokana na mahakama kuu kufuta matokeo ya upigaji kura uliofanyika Agosti 8 kumeleta athari mbaya kwa shughuli za biashara nchini humo, na ukuaji mdogo wa uchumi pia unatokana na ukame ulioathiri sekta ya kilimo ambayo ni nguzo ya uchumi wa Kenya.

    Tume huru ya uchaguzi na mipaka imeomba takriban dola za Marekani milioni 125 kwa ajili ya kurudiwa uchaguzi wa rais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako