• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai kushirikiana zaidi katika vita dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-09-17 18:06:31

    Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai itaendelea kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi, ufarakanishaji na misimamo mikali.

    Habari hizo zimetolewa kwenye mkutano wa 31 wa kamati ya idara za kupambana na ugaidi wa kikanda za nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai, zikiwemo China, Russia, India, Pakistan, Kazakhstan na nyinginezo.

    Mkutano huo ulijumuisha hali ya ushirikiano wa jumuiya hiyo dhidi ya ugaidi katika kipindi kilichopita, na kujadili matokeo ya semina ya mapambano dhidi ya ugaidi, ufarakanishaji, misimamo mikali kwa njia ya mtandao wa Internet, na mazoezi ya pamoja ya kupambana na ugaidi, kutafiti hali ya utekelezaji wa hatua za pamoja za kudadisi na kukata njia ya kuhamisha magaidi, na kuamua kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako