• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Sudan lakanusha kushambulia eneo la waasi katika jimbo la Blue Nile

    (GMT+08:00) 2017-09-17 18:27:47
    Jeshi la Sudan lakanusha kushambulia eneo la waasi katika jimbo la Blue Nile

    Jeshi la Sudan jumamosi limesisitiza ahadi zake za kusitisha mapigano katika maeneo yote ya migogoro, na kukanusha madai ya waasi kwamba jeshi hilo lilishambulia eneo lao katika jimbo la Blue Nile.

    Siku moja kabla, kundi la waasi la harakati ya ukombozi wa watu wa Sudan (SPLM) mkoa wa kaskazini lilishutumu jeshi la serikali kwa kushambulia sehemu yake katika jimbo hilo.

    Msemaji wa jeshi la Sudan Ahmed Khalifa Al-Shami ameeleza kuwa, jeshi la Sudan linasisitiza tena ahadi zake za kusitisha mapigano dhidi ya waasi.

    Amesema shutuma ya waasi ina kusudi la kuharibu ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Sudan huko Washington.

    Mwezi Julai, Rais wa Sudan Omar al-Bashir alitangaza kusimamisha mapigano katika maeneo yote ya migogoro kwa miezi mitatu hadi Oktoba mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako