• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapambano yaliyotokea nchini Libya yasababisha vifo vya watu watano

    (GMT+08:00) 2017-09-18 09:22:07

    Mapambano kati ya vikosi vya usalama vya Libya katika mji wa magharibi wa Sabratha yamesababisha vifo vya watu watano na wengine wanane kujeruhiwa.

    Habari zinasema mapambano hayo yametokea kati ya wana usalama wa kikosi cha kupambana na kundi la IS na wapiganaji wa baraza la mji wa Sabratha. Licha ya kuwa mapambano kati ya pande mbili yalisimamishwa baada ya upatanishi wa wazee, milio ya risasi iliendelea kusikika.

    Habari pia zinasema umoja wa mataifa utatuma wana usalama 200 kulinda ofisi za tume ya umoja huo nchini Libya. Msemaji wa tume ya umoja wa mataifa nchini Libya amesema wana usalama hao watakwenda Libya kwa vikundi, ikiwa ni hatua ya mwanzo kwa Umoja wa mataifa kurudisha shughuli zake Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako