Habari kutoka Somalia zimethibitisha kuwa ofisa mwandamizi wa idara ya ujasusi ya Somalia Bw Mohamud Hassan Moalim ameuawa, na walinzi wake wamejeruhiwa katika shambulizi la ufyatuaji risasi lililotokea eneo la Dharkenlay mjini Mogadishu.
Waasi kutoka Kundi la Al-Shabaab wanatuhumiwa kuhusika na shambulizi hilo, lakini hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambilizi hilo.
Kamishna wa eneo la Kahda Bw Mohamed Ismael amethibitisha kwamba Bw Mohamud Hassan Moalim amefariki kutokana na kujeruhiwa vibaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |