• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande zote za Palestina zafurahia Kundi la Hamas kuondoa kamati ya utawala kwenye ukanda wa Gaza

    (GMT+08:00) 2017-09-18 09:46:55

    Kundi la Hamas la Palestina limetangaza kuondoa kamati ya utawala iliyoko ukanda wa Gaza na kukubali kufanya uchaguzi mkuu.

    Katibu mkuu wa kamati ya mapinduzi ya Kundi la Fatah Bw Majid Fatyani amefurahia uamuzi wa Kundi la Hamas, na kuutaja kuwa ni hatua ya kiutendaji katika kusimamisha mgawanyiko wa taifa.

    Ofisa wa Kundi la Fatah anayeshughulikia mambo ya maafikiano Bw Azzam Ahmad hivi sasa anaongoza ujumbe wa kundi hilo kuzungumza na upande wa Misri kuhusu maafikiano ya mambo ya ndani ya Palestina, pia amesema Kundi la Fatah litafanya mkutano na Hamas, ili kuhimiza umoja wa taifa.

    Mbali na hayo, pande husika za Palestina ikiwa ni pamoja na makundi mengine pia yametoa taarifa kukaribisha uamuzi uliotolewa na Kundi la Hamas.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako