• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani inaweza kubaki kwenye Mkataba wa Paris kama masharti yake yakifuatwa

    (GMT+08:00) 2017-09-18 09:49:54

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson amesema Marekani inaweza kuendelea kubaki kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kama masharti yake yatafuatwa.

    Kauli ya Bw Tillerson inalingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje kuwa Marekani iko wazi kujiunga tena katika Mkataba wa Paris kama itanufaisha mambo yake ya biashara, wafanyakazi, wananchi pamoja na walipa kodi wake.

    Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza uamuzi wa Marekani kujiondoa kutoka Mkataba wa Paris June 1, akitaja wasiwasi wake kuhusu changamoto zinazoletwa na mkataba huo kwa uchumi wa Marekani. Hata hivyo atafuata kanuni iliyowekwa na mkataba huo kwamba Marekani haitajiondoa kabla ya mwezi Novemba mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako