• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiwango cha juu cha umaskini chasababisha ongezeko la uhalifu Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2017-09-18 09:50:23

  Kiwango cha uhalifu unaohusisha uporaji wa kutumia silaha kwenye barabara kuu, uvunjaji wa nyumba na udokozi umekuwa ukiongezeka kutokana na kiwango cha juu cha umaskini na udhaifu wa utekelezaji wa sheria mjini Juba, Sudan Kusini.

  Tangu mapigano mapya yalipuke mwaka jana mjini Juba, uhalifu mbalimbali umeongezeka kutokana na msukosuko wa kiuchumi ikiwa ni pamoja na mfumuko wa bei ambao ulisababisha idadi kubwa ya watumishi wa umma na mashirika ya utekelezaji wa sheria kutolipwa mshahara katika miezi minne iliyopita.

  Msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema jeshi hilo limeimarisha doria ili kuzuia uhalifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako