• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yawarai wawekezaji wa Qatar

    (GMT+08:00) 2017-09-18 18:07:12

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema nchi hiyo inaingia kwa haraka kwenye daraja la uchumi wa wastani huku ikiwa na nafasi nyingi za uwekezaji kwenye sekta za kilimo, viwanda na utoaji wa huduma.

    Museveni ameyasema hayo wakati akikutana na ujumbe wa maafisa wa hazina ya uwekezaji kutoka Qatar.

    Rais Museveni amekutana na ujumbe huo mjini NewYork Marekani ambako kunafanyika mkutano wa 72 wa baraza kuu la umoja wa Mataifa.

    Kiongozi wa ujumbe huo Sheikh Abdulla amesema wangependa kuwekeza kwenye sekta za kawi, miundo mbinu na huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako