• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kuimarika bei ya Tungsten afueni kwa Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-09-18 18:07:34

    Ripoti za masoko wiki jana zimeonyesha kwamba bei ya madini ya tungsten, ambayo ni mojawepo wa yale Rwanda inayozalisha kwa wingi imepanda

    Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji cha Rwanda Jean Malik Kalima, amesema kuimarika kwa bei ni ishara zuri ikizingatiwa uwekezaji mkubwa uliowekwa kwenye sekta hiyo.

    Tungsten, ambayo pia hujulikana kama wolfram, ni ngumu, adimu na inatumika kwa njia mbalimbalikwani inadumu.

    Tani moja ya tungsten sasa inauzwa kwa kati ya dola 310 na 345 ikilinganishwa na bei ya miezi kadhaa iliopita ya dola 200.

    Kalima amesema baadhi ya wawekezaji ya kigeni ambao walikuwa wameanza kuondoka sasa wameanza kurejea kutokana na kuimarika kwa bei.

    Madini yako kwenye nafasi ya pili miongoni mwa bidhaa inazouza Rwanda kwenye masoko ya nje mwaka 2014 yakiwa yameiletea nchi hiyo dola milioni 210.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako