• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya soko la nyumba nchini China yaendelea kutulia

    (GMT+08:00) 2017-09-18 18:41:26

    Soko la nyumba nchini China limeendelea kuonyesha ishara ya kutulia wakati bei ya nyumba ikishuka au kukua kwa taratibu katik miji mikubwa nchini humo.

    Idara ya Takwimu ya Taifa imesema, kati ya miji 70 iliyofanyiwa utafiti mwezi Agosti, kasi ya kupanda kwa bei za nyumba imeshuka katika miji 15 mikubwa ikilinganishwa na mwaka jana. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, bei za nyumba mpya zilishuka au kubaki zilizoko katika miji 13 mwezi uliopita.

    Bei ya nyumba katika miji 15 mikubwa ilishuka kutoka asilimia 1.3 mpaka asilimia 6.6 mwezi Agosti ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako