• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Afghanistan lawaua wapiganaji 6 wa kundi la Taliban kaskazini mwa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2017-09-18 20:27:16

    Wapiganaji zaidi ya 6 wa kundi la Taliban wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa kufuatia operesheni ya jeshi la Afghanistan ya kujibu mashambulizi iliyofanywa na kundi hilo katika mkoa wa Baghlan ulioko kaskazini mwa nchi hiyo.

    Mkuu wa polisi wa mkoa huo Jenerali Ukramuddin Sari amesema, shambulizi hilo lilitokea jana jioni, wakati kundi la Taliban liliposhambulia maeneo ya Bagh-e-Shamal na Surkh Kotal ya mji mkuu wa mkoa huo Pul-e-Khumri, lakini walikimbia baada ya jeshi la serikali kujibu shambulizi hilo.

    Ameongeza kuwa raia watatu wamejeruhiwa kutokana na shambulizi la mizinga ya wapiganaji hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako