• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria ladhibiti asilimia 75 ya Deir al-Zour

    (GMT+08:00) 2017-09-19 08:59:25

    Shirika la uangalizi wa haki za binadamu nchini Syria limesema, jeshi la Syria na washirika wake wanadhibiti asilimia 75 ya mji mkuu wa mkoa wa Deir al-Zour, mashariki mwa Syria, baada ya mapambano na kundi la IS,

    Mapema jana, chanzo cha habari kiliambia shirika la habari la China, Xinhua kuwa, kituo cha jeshi la anga cha Deir al-Zour kimerejesha operesheni zake.

    Amesema ndege za kivita za jeshi la Syria zimeanza kushiriki kwenye operesheni dhidi ya wapiganaji wa kundi la IS.

    Wakati huo huo kutokana na uungaji mkono wa jeshi la anga la Russia, vikosi vya Syria vimefika kando ya Mto Euphrates huko Deir al-Zour.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako