• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama kuu ya Iraq yaliagiza jimbo la wakurd lisimamishe upigaji kura za maoni

    (GMT+08:00) 2017-09-19 09:09:24

    Mahakama kuu ya Iraq imelitaka jimbo la wakurd lisimamishe upigaji kura za maoni uliopangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya habari ya mahakama kuu ya Iraq imesema wajumbe wote wa mahakama kuu jana walikutana kujadili suala la upigaji kura za maoni katika jimbo la wakurd na maeneo mengine. Baada ya mkutano wao, mahakama ilitoa agizo la kusimamisha mchakato wa upigaji kura za maoni.

    Mwezi Juni mwaka huu jimbo la wakurd la Iraq lilitangaza kupiga kura za maoni kuhusu kujitenga na Iraq mwezi huu, kitendo ambacho kimepingwa vikali na serikali kuu ya Iraq, Uturuki na Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako