• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hospitali ya China yapata umaarufu Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-09-19 09:15:39

    Hospitali ya Urafiki wa China iliyoko karibu na Uwanja wa Ndege wa Juba, Sudan Kusini, ni moja kati ya mashirika matatu ya matibabu yanayoendelea kutoa huduma baada ya mapigano mapya kutokea Mwezi Julai mwaka jana.

    Wananchi wengi wa Sudan Kusini wanachagua hospitali hiyo binafsi yenye wataalamu wa kichina, na madaktari wenye uzoefu wa Sudan Kusini, na wale wanaotoka Afrika Mashariki kwa ajili ya kutibu magonjwa yote yasiyo ya kuambukiza na magonjwa sugu.

    Mkurugenzi wa hospitali hiyo Bw. Ma Ning amesema hospitali hiyo inashughulikia magonjwa ya homa za matumbo na malaria, lakini pia inajivunia kwa kufanya upasuaji wa kwanza wa jicho nchini humo mwezi Septemba. Ameongeza kuwa wakati wa vurugu zilizoibuka mwaka 2016, waliwatibu askari na wananchi waliojeruhiwa kutokana na mapambano kati ya jeshi la serikali SPLA na kundi la waasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako