• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi yaitaka DRC kuchunguza mauaji ya wakimbizi wa Burundi nchini humo

    (GMT+08:00) 2017-09-19 09:17:05

    Burundi imeitaka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kutoa maelezo kuhusu mauaji ya wakimbizi wasiopungua 30 wa Burundi wiki iliyopita nchini humo.

    Msemaji wa serikali ya Burundi Bw Philippe Nzobonariba amesema, baada ya kupewa habari kuhusu kuuawa kwa wakimbizi hao kutokana na mapambano kati yao na jeshi la DRC, serikali ya Burundi kupitia wizara yake ya mambo ya nje iliitaka DRC kuchunguza mauaji hayo na kutaja ni nani wanahusika.

    Pia amesema ofisi ya shirika la kuhudumia wakimbizi ya umoja wa mataifa UNHCR nchini DRC, pamoja na kikosi cha kulinda utulivu cha Umoja wa Mataifa nchini humo pia wanapaswa kutoa maelezo kuhusu tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako