• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaharakisha kuendeleza shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo

    (GMT+08:00) 2017-09-19 17:46:37

    Wizara ya kilimo, kamati ya maendeleo na mageuzi, na wizara ya fedha nchini China leo zimetoa waraka, ukisema China itaharakisha kuendeleza shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo, na kujitahidi kuongeza nafasi ya shughuli hizo katika thamani ya uzalishaji mali wa kilimo.

    Shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo ni shughuli za huduma maalumu za mfululizo kwa ajili ya uzalishaji wa kilimo, ambazo ni pamoja na kununua malighafi za kilimo, kutoa mashine za kupanda na kuvuna mazao, kutafiti ardhi na uwekaji wa mbolea, kuhifadhi mazao yaliyokauka, kuhifadhi mazao mabichi, na huduma za habari.

    Mkurugenzi wa idara inayoshughulikia mfumo na uendeshaji wa kilimo vijijini iliyo chini ya wizara ya kilimo ya China Bw. Zhang Hongyu leo kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, waraka uitwao "maoni ya kuelekeza namna ya kuharakisha kuendeleza shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo", umepanga kazi muhimu na hatua zipaswazo kwa idara husika za serikali katika kuelekeza mashirika ya aina mbalimbali ya huduma kupanua shughuli, kuvumbua njia mpya, na kuinua kiwango cha huduma zao. Anasema,

    "Waraka huo unahimiza shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo kufuata kanuni za kulinganisha mahitaji ya soko, kuvumbua njia mpya ya maendeleo, na kuzingatia sifa ya huduma, na kuchukua kuhudumia kilimo na wakulima kuwa ni msingi, na kukuza shughuli ya kimkakati ya kuhudumia uzalishaji wa kilimo kuwa ni lengo, na kuzingatia mageuzi ya muundo wa mazao ya kilimo, ili kuendeleza huduma za ngazi na aina tofauti kwa ajili ya uzalishaji wa kilimo, na kusukuma mbele ujenzi wa kilimo cha kisasa katika sekta mbalimbali."

    Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kilimo, shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo zinaendelea kwa haraka, hadi sasa nchini China kuna mashirika ya shughuli hizo zaidi ya milioni 1.15, yanayohudumia sekta mbalimbali za kilimo, zikiwemo upandaji, mifugo na uvuvi. Lakini mashirika hayo ni madogo, hayana uwezo wa kutosha wa kuhudumia shughuli za kilimo vijijini ambazo zinakabiliwa na changamoto ya kupungua na kuzeeka kwa watu.

    Waraka huo unapendekeza kwa kutumia miaka mitano, China itaongeza kidhahiri nafasi ya shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo katika thamani ya uzalishaji mali wa kilimo, kuinua kiwango chake na kukamilisha mtandao mzuri unaoweza kuhudumia vizuri uzalishaji wa kilimo katika sekta mbalimbali. Bw. Zhang Hongyu amesema huduma hizi zinapaswa kuhusisha mambo yote,

    "Huduma hizo ni pamoja na utoaji wa habari za mahitaji za soko, malighafi za uzalishaji, teknolojia haswa zile zisizoleta uchafuzi kwa mazingira, na shughuli baada ya mavuno. Zaidi ya hayo, masuala ya mashine, utengenezaji mpya na mauzo ya mazao pia yanatakiwa kutatuliwa."

    Waraka huo pia umesema baadaye China itaeneza amana za shughuli za uzalishaji wa kilimo kwa nguvu zaidi, na kutafuta na kuvumbua mfumo wa huduma za kueneza teknolojia za kilimo. Hivi sasa shughuli za kuhudumia uzalishaji wa kilimo zinavutia uwekezaji vijijini, na baadaye serikali itahimiza zaidi uwekezaji katika shughuli hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako