• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Naivas na Carrefour yawania kuchukua nafasi Thika Road Mall

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:20:02

    Maduka makuu ya Naivas na Carrefour yanawania kuchukua nafasi ya duka lililofungwa la Nakumatt Thika Road Mall (TRM).

    Nakumatt, ilitoa tangazo Jumatatu kwamba imefunga duka lake hilo la TRM ili kufanya hesabu za ndani lakini wataalam wa kifedha wanasema kufungwa kwake kunatokana na masaibu ya kifedha yanayokumba maduka hayo.

    Mkurugenzi wa jumba la TRM Bashir Dalvi,amesema wanafanya mazungumzo na Nakumatt ili waondoke kwenye nafasi hiyo kwani wamedaiwa esa nyingi za kodi.

    Naye mkurugenzi wa oparesheni wa maduka ya Naivas, Willy Kimani amesema wangependa sana kuchukua nafasi hiyo ya TRM.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako