• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Vijana Rwanda watakiwa kujihusisha na biashara

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:20:23

    Waziri wa vijana wa Rwanda Rosemary Mbabazi, ametoa wito kwa viajana nchini humo kukumbatia ujasiriamali na kukuza amani kwa ajili ya maendeleo endelevu.

    Mbabazi ameyasema hayo wakati wa siku ya kimataifa ya vijana wilayani Gicumbi ambayo maudhui yake yalikuwa ni " Viajna kukumbatia amani kama nguzo ya maendeleo".

    Alisema siku ya kimataifa ya vijana inatambua wajibu wao katika ujenzi wa taifa huku akiwataka kujiepusha na madawa ya kulevya au mizozo ya kijamii.

    Mratibu wa kitaifa wa baraza la vijana nchini humo Jean-Damascene Ahishakiye, alisema viaja katika wilaya hiyo ya Gicumbi, wameanzisha makundi ya kukabili matumizi ya madawa ya kulevya na pia kuelimisha jamii kuhusu athari zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako