• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Ujenzi wa eneo la kupakua makasha Mombasa kuanza Januari

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:20:51

    Awamu ya pili ya ujenzi wa eneo la kupakua makasha kwenye bandari ya Mombasa unatarajiwa kuanza Januari mwakani.

    Hii ni baada ya mamlaka ya bandari nchini humo KPA, kupata mkopo wa shilingi bilioni 35 kutoka Japan ili kukamilisha mradi huo.

    Mkurugenzi wa KPA, Catherine Mturi-Wairi, amesema mchakato wa kutoa kandarasi utaanza hivi karibuni .

    Awamu hiyo ya pili itawezesha bandari hiyo kupakua makasha 450,000 kwa mwaka.

    Wakati huo huo waziri wa uchukuzi nchini Kenya James Macharia amesema serikali inatafuta fedha zaidi ili kujenga kituo cha kisasa na kikubwa zaidi cha mafuta ili kuchukua mahali pa kile cha Kipevu mjini Mombasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako