• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la chini la bunge la Marekani lapitisha mswada wa kuidhinisha bajeti ya ulinzi wa taifa

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:39:07

    Baraza la chini la bunge la Marekani limepitisha mswada unaoidhinisha bajeti ya ulinzi wa taifa yenye thamani ya dola bilioni 700 za kimarekani kwa kura 89 za ndiyo dhidi ya kura 8 za hapana.

    Kwa mujibu wa mswada huo, kuanzia mwaka wa fedha wa 2018 utakaoanza Oktoba Mosi, thamani ya matumizi ya ulinzi wa taifa wa Marekani utakuwa ni dola bilioni 700 za kimarekani, ambapo fedha hizo zitatumiwa katika manunuzi ya wizara ya ulinzi na malipo ya wanajeshi, na nyingine zitatumika katika operesheni za jeshi la Marekani nchini Afghanistan, Iraq na Syria.

    Habari nyingine zinasema, waziri wa ulinzi wa taifa wa nchi hiyo Bw. James Mattis amethibitisha kuwa jeshi la Marekani litaongeza askari zaidi ya elfu 3 nchini Afghanistan, ili kuimarisha uwezo wa jeshi la serikali la Afghanistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako