• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti yaonesha kuwa Misri imekuwa nchi nzuri zaidi ya uwekezaji barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:45:51

    Benki ya Biashara ya Afrika Kusini imetoa mwongozo wa uwekezaji barani Afrika mwaka 2018 ukionesha kuwa, kutokana na nguvu bora ya ongezeko la uchumi, Misri imeizidi Afrika Kusini na kuwa nchi nzuri zaidi ya uwekezaji barani Afrika.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Kusini kuchukua nafasi ya pili katika orodha ya nchi 10 bora kwa uwekezaji barani Afrika tangu Benki hiyo ianze kutoa mwongozo wa uwekezaji barani Afrika katika miaka 7 iliyopita. Kwa mujibu wa mwongozo huo, Morocco, Ethiopia na Kenya zimekuwa nafasi ya 3 hadi 6.

    Mwongozo huo pia umesema, ongezeko imara la uchumi ni chanzo kikuu cha Misri kushika nafasi ya kwanza, huku wasiwasi unaotokana na msukosuko wa sera na utawala wa serikali ya Afrika Kusini zikiathiri imani za wawekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako