• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu elfu 70 hawana makazi kutokana na vita vya kikabila nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:59:48

    Zaidi ya watu elfu 70 wa kabila la Oromo nchini Ethiopia wamekimbia makazi yao katika mkoa wa Somali nchini humo baada ya mapigano yaliyodumu kwa wiki moja dhidi ya Wasomali wazawa ambayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa.

    Waziri wa masuala ya mawasiliano ya serikali ya Ethiopia Negeri Lencho amesema, serikali yake imeunda kikosi kazo ili kutoa misaada kwa watu waliokimbia makazi yao. Ameongeza kuwa hali ya utulivu imeanza kurejea katika eneo hilo licha ya vurugu kidogo katika mpaka kati ya mikoa ya Oromia na Somali.

    Mikoa hivyo miwili mikubwa nchini Ethiopia imekuwa na mvutano kuhusu mpaka wa mikoa hiyo kwa karibu miongo miwili. Kama sehemu ya kutuliza hali ya eneo hilo, serikali kuu ya Ethiopia jumamosi ilitangaza kuwa barabara zinazopita kwenye mikoa hiyo zitalindwa na polisi, na wanajeshi wa serikali za mikoa hiyo wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo ya mipaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako