• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabalozi wa nchi za nje nchini Kenya wawataka Wakenya waondoe chuki na vurugu kabla ya marudio ya uchaguzi wa rais

    (GMT+08:00) 2017-09-19 20:47:35

    Mabalozi wa nchi 15 za Magharibi nchini Kenya wametoa wito kwa raia wa Kenya kujizuia na vitendo na kauli zinazochochea chuki na vurugu kabla ya kutolewa kwa hukumu kamili ya Mahakama Kuu kuhusu uchaguzi wa urais.

    Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Nairobi, mabalozi hao wamesema ingawa wanaunga mkono uhuru wa kujieleza, mashambulizi na maneno yasiyo na msingi ni lazima yaachwe, na viongozi wa pande zote wahakikishe kuwa jambo hilo linafanyika.

    Wanadiplomasia hao wamesema Kenya inapaswa kuwa makini katika kuandaa uchaguzi mpya, ambao, kwa kuendana na amri ya Mahakama na Katiba, ni lazima uandaliwe na Tume ya Uchaguzi na kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako