• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tunisia na mkuu wa jeshi la taifa la Libya wajadili kuhusu mapambano nchini Libya

    (GMT+08:00) 2017-09-19 20:58:16

    Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia amekutana na jenerali Khalifa Haftar anayedai kuwa mkuu wa jeshi la taifa la Libya, na kujadili kuhusu utatuzi wa mapambano ya Libya.

    Serikali ya umoja wa taifa ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa inaendeshwa magharibi mwa nchi hiyo, ambayo makao makuu yake yako huko Tripoli, huku serikali ya upinzani inayoungwa mkono na jeshi ambalo Jenerali Haftar anadai kuwa ni la Libya iko huko Tobruk. Jeshi hilo limedhibiti sehemu nyingi za mashariki na kusini mwa nchi hiyo na kutaka kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

    Rais Essebsi amesema, ziara ya Jenerali Haftar ni sehemu ya juhudi za Tunisia kuchangia utatuzi wa mapigano ya Libya kupitia makubaliano kati ya pande husika.

    Katika mkutano huo, rais huyo amewataka Walibya kurejesha mazungumzo, makubaliano na ujenzi tena wa serikali ya nchi hiyo, huku akiongeza kuwa utulivu wa Tunisia unategemea utulivu wa Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako