• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wenye silaha wafunga bomba la mafuta magharibi mwa Libya

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:19:50

    Watu wenye silaha wasiojulikana wamefunga bomba la mafuta katika mji wa Zawiya, magharibi mwa Libya, linalosafirisha mafuta hadi mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli. Taarifa iliyotolewa na kampuni ya mafuta ya taifa la Libya inasema kikundi cha watu wenye silaha waliingia kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta mjini Zawiya na kuwalazimisha wafanyakazi kukata utoaji wa mafuta kwa Tripoli. Taarifa inasema vitendo hivyo vya hujuma vinavyolenga kuchochea vurugu vitaongeza mateso kwa wananchi, na kusisitiza kuwa kampuni hiyo itachukua hatua za kisheria kama bomba hilo litaendelea kufungwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako