• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yalifungia jarida la Mwanahalisi kwa miaka miwili

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:27:28

    Serikali ya Tanzania imelifungia jarida la Mwanahalisi kwa muda wa miaka miwili kutokana na kuchapisha habari za uchochezi na kushindwa kufuata kanuni za taaluma ya uandishi wa habari.

    Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo ya Tanzania Dk Hassan Abbas amesema, marufuku hiyo ambayo ni kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha sheria mpya ya huduma za habari, pia inalihusisha toleo kwenye mtandao wa internet.

    Baadhi ya sababu za kufungiwa kwa jarida hilo zilizotajwa ni pamoja na kuitaja Ikulu ya Tanzania kuhusika na ufisadi, bila kuwa na ukweli.

    Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa serikali ya Tanzania kujaribu kulifungia jarida la Mwanahalisi. Mwaka 2012 serikali ilichukua hatua kama hiyo, lakini wahariri wake walipinga mahakamani, na mahakama kuamuru lisifungiwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako