• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama kuu ya Kenya yalaani kushambuliwa na wanasiasa wakati kampeni za uchaguzi wa Rais zikipamba moto

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:27:50

    Mahakama kuu ya Kenya imelaani kauli za kuishambulia kutoka kwa wanasiasa wa Kenya na kusema itaendelea kutekeleza majukumu yake bila hofu na bila upendeleo.

    Jaji Mkuu wa Kenya Bw David Maraga amesema tangu mahakama kuu ifute matokeo ya uchaguzi wa rais, mahakama hiyo imekuwa ikishambuliwa zaidi, hadi kufikia hatua ya kuwepo kwa maandamano nje ya jengo la mahakama kuu ya Kenya. Jana pia Rais Kenyatta aliwataja majaji wanne waliofuta ushindi wake kuwa ni wahuni, na kusema akichaguliwa kuwa rais atasafisha mahakama.

    Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa maelezo ya kina ni kwanini iliamua kufuta matokeo ya uchaguzi wa Rais. Mahakama ilitakiwa kutoa maelezo hayo jana, lakini kutokana na maandamano yaliyokuwa yanafanyika nje ya mahakama hiyo, uamuzi huo uliahirishwa hadi leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako