• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miili ya watanzania 14 waliofariki kwenye ajali ya barabarani Uganda yasafirishwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:49:49

    Naibu msemaji wa serikali ya Uganda Bw. Shaban Batariza amesema, miili ya watanzania 14 waliofariki kwenye ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa jumapili kwenye eneo la Mpigi katikati ya Uganda, imesafirishwa kwenda Tanzania.

    Bw. Batariza amesema askari polisi wa Uganda na Tanzania wameshirikiana kurejesha miili hiyo kwa ajili ya mazishi.

    Watu 14 walikufa na wengine 17 walijeruhiwa baada ya lori moja kugongana na basi aina ya Coaster kwenye barabara ya mwendo kasi ya Kampala-Masaka huko Katonga.

    Ajali hiyo ilitokea wakati watu hao walipokuwa wanarudi nyumbani Tanzania baada ya kushiriki kwenye sherehe ya harusi ya ndugu yao mjini Kampala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako