• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yapitisha mkakati wa COMESA wa kuendeleza viwanda

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:50:15

    Mkurugenzi wa sekta ya viwanda katika Jumuiya ya soko la pamoja la Afrika Mashariki na Kusini COMESA Bw.Thierry Mutombo amesema, Zambia imekuwa moja ya nchi wanachama 15 wa jumuiya ya COMESA, zilizopitisha mkakati wa kuendeleza viwanda wa jumuiya hiyo, unaolenga kuharakisha mendeleo ya viwanda kwenye kanda hiyo.

    Mkakati huo uliopitishwa na Baraza la mawaziri la COMESA mwaka 2015, unathibitisha hatua muhimu kwenye ngazi za kikanda na kitaifa, kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya viwanda katika kanda hiyo.

    Wiki iliyopita, mawaziri wa viwanda wa nchi wanachama wa COMESA walikutana Lusaka Zambia, ambapo walifanya marekebisho ya mwisho kuhusu waraka wa mkakati huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako