• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtuhumiwa wa tatu wa mlipuko uliotokea London akamatwa

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:54:03

    Polisi wa Uingereza wametangaza kumkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 25 mjini Newport, Wales akiwa mtuhumiwa wa tatu wa mlipuko uliotokea Ijumaa kwenye kituo cha subway magharibi mwa London.

    Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa huyo alikamatwa jana jioni, na nyumba anayeishi sasa inafanyiwa uchunguzi.

    Msemaji wa Scotland Yard amesema operesheni hiyo ilifanyika kutokana na amri ya kituo kikuu cha kupambana na ugaidi cha Met, kwa kushirikiana na Polisi ya Gwent na kikosi maalumu cha kupambana na itikadi kali na ugaidi cha Wales WECTU.

    Kabla ya hapo, watu wengine wawili wenye umri wa miaka 18 na 21 wanaotuhumiwa kuhusika na mlipuko huo pia walikamatwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako