• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yathibitisha watu 39 wauawa nchini DRC

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:54:27

    Taarifa iliyotolewa na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR imesema watu wasiopungua 39 waliuawa na wengine 94 kujeruhiwa kwenye shambulizi nchini DRC wiki iliyopita.

    Shirika hilo limesema shambulizi hilo lilitokea baada ya askari wa DRC kuwafyatulia risasi waandamanaji wa Burundi katika sehemu mashariki mwa DRC, wengi wao wakiwa ni wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi.

    Habari zinasema waandamanaji hao waliandamana kiamani baada ya kikundi kimoja cha warundi kukamatwa na mamlaka za DRC na kusababisha hofu yao ya kufukuzwa kurudi Burundi.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vifo hivyo ni pamoja wanaume na wanawake warundi, mtoto mmoja na askari mmoja wa DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako