• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 216 wafariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Mexico

    (GMT+08:00) 2017-09-20 18:18:28
    Watu 216 wamefariki baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.1 kwenye kipimo cha Richter kutokea katikati ya Mexico jana.
    Tetemeko hilo liliangusha nyumba kadhaa, kupasua mabomba ya gesi na kusababisha ajali za moto, na hivyo kuwafanya maelfu ya watu kikimbilia barabarani kwa woga.
    Rais Enrique Pena Neto amewataka wananchi kuwa watulivu, na ameziagiza hospitali zote kutoa matibabu kwa majeruhi wa tetemeko hilo. Amesema kipaumbele kwa sasa ni kuendelea kufanya kazi ya kuwaokoa watu waliokwama kwenye vifusi vya majengo yaliyobomoka.
    Mkuu wa idara ya ulinzi wa raia nchini humo Luis Felipe Puente amesema, idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa kuwa watu wengi bado wamekwama kwenye vifuzi vya majengo yaliyobomoka.
    Waziri wa elimu Aurelio Nuno Mayer ametangaza kusitisha masomo kwa shule zote kwenye maeneo yaliyoathirika na tetemeko hilo mpaka itakapotangazwa hapo baadaye.
    Habari nyingine zinasema, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang hapa Beijing ametoa salamu za rambirambi kwa vifo vilivyosababishwa na tetemko la ardhi nchini Mexico. Pia amesema, China ina imani kuwa wananchi wa Mexico wataweza kujenga tena makazi yao mapema.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako