• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria mazungumzo yasiyo rasmi ya ngazi ya juu ya suala la mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-09-20 18:29:41

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amehudhuria mazungumzo yasiyo rasmi ya ngazi ya juu kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa yaliyofanyika jana mjini New York, Marekani.

    Katika mazungumzo hayo, Wang Yi amesema kuwa tangu kutekelezwa rasmi kwa makubaliano ya Paris mwezi Novemba mwaka jana, jumuiya ya kimataifa imeingia katika kipindi muhimu cha kufanya juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Nchi zote zinapaswa kutekeleza kihalisi ahadi zilizotolewa na viongozi wao huko Paris, na kushikilia msimamo wa kufanya ushirikiano kwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunganisha kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutekeleza kihalisi ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

    Aidha Bw. Wang Yi alikutana na naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Namibia Bw. Netumbo Nandi-Ndaitwah katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Bw. Wang Yi alisema China inapenda kuimarisha mawasiliano kati viongozi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako