• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Madagascar zasaini mradi wa kuwawezesha watu wenye mtoto wa jicho kuona tena

    (GMT+08:00) 2017-09-20 18:30:31

    Mradi wa kuwawezesha watu kuona tena unaofanyika kwa msaada wa China nchini Madagascar umesainiwa jana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo.

    Hafla ya kusainiwa kwa mradi huo ilihudhuriwa na waziri wa afya wa Madagascar Bw. Lalatiana Andriamanarivo,balozi wa China nchini Madagascar Bw. Yang Xiaorong na wajumbe zaidi 40 wa sekta ya afya na matibabu wa China na Madagascar.

    Bw. Andriamanarivo amesema, ugonjwa wa mtoto wa jicho ni mojawapo wa magonjwa yanayosababisha upofu nchini Madagascar. Amesema wataalamu wa magonjwa ya macho kutoka China watafanya upasuaji bure kwa watu 200 wenye mtoto wa jicho nchini Madagascar na pia wataleta misaada ya vifaa vya matibabu kwa hospitali za huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako