• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia kuchukua hatua maalum kama Marekani itajitoa kutoka makubaliano ya makombora ya masafa ya kati

    (GMT+08:00) 2017-09-20 18:36:55

    Naibu mwenyekiti wa kwanza wa kamati ya ulinzi na usalama ya Russia Bw. Frants Klintsevich amesema, Russia itaweza kuchukua hatua maalumu kama Marekani itaamua kujitoa katika makubaliano ya makombora ya masafa ya kati INF.

    Bw. Klintsevich amesema, hatua hiyo itaandaliwa ili kuhakikisha usalama wa Russia, ambayo ni pamoja na uwezekano wa kutumia mifumo yake ya ulinzi wa anga. Pia amesema, kama Marekani itajitoa kwenye makubaliano hayo, Russia itatengeneza silaha zinazofanana na makombora ya masafa mafupi na ya kati ambayo yatafika kilomita elfu 1.5.

    Bw. Klintsevich amesema hayo baada ya baraza la juu la bunge la Marekani kupitisha sera mpya ya ulinzi, ambayo inaidhinisha wizara ya ulinzi kuanza kuendeleza makombora ya aina mpya yenye masafa ya kiliomita 500 hadi 5500.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako