• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zambia yatetea kununua magari ya zimamoto kwa bei kubwa kupita kiasi

    (GMT+08:00) 2017-09-20 18:39:53

    Serikali ya Zambia imetetea uamuzi wake wa kununua magari 42 ya zimamoto kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 42, na kusema zabuni ya ununuzi huo ilifanyika kwa njia ya wazi.

    Wiki iliyopita, makamu wa rais Inonge Wina alizindua magari hayo lakini bei iliyotumika kuyanunua imelalamikiwa sana, huku wakosoaji na vyama vya upinzania vya siasa wakiuliza kwa nini serikali imenunua magari hayo kwa gharama ya dola milioni moja za kimarekani kwa kila gari.

    Lakini waziri wa Serikali za Mitaa Vincent Mwale amesema, zabuni ya kununua magari hayo ilifikiwa baada ya uchunguzi wa kina wa watu wote walioomba zabuni hiyo, na wataalam wa zimamoto waliohusishwa katika mchakato wa manunuzi walitaka vifaa maalum vya ubora wa juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako