• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapokea mkopo wa Ksh15.5bn kufadhili mradi wa kuunganisha umeme

    (GMT+08:00) 2017-09-20 20:53:54

    Serikali ya Kenya imepokea mkopo wa shilingi bilioni 15.5 kutoka kwa benki ya dunia kufadhili mradi wa kuunganisha umeme katika kaunti za maeneo kame. Fedha hizo zitatumiwa kununua paneli za jua ambazo zitasaidia kuunganisha umeme kwa nyumba elfu 690. Nyumba hizo ni katika kaunti 14 ambazo zimetajwa kuwa kaunti za maeneo kame.

    Waziri wa nishati Bw Patrick Njoroge amesema fedha hizo zitahakikisha kuwa lengo la serikali la kuunganisha kila nyumba na umeme linafikiwa. Ameongeza kuwa wataanza na kaunti za Moyale, Garissa na pOKOT mAGHARIBI. Amesema hivi sasa nyumba milioni 6.2 tayari zimeunganishiwa umeme kote nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako