• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Bei ya kahawa yaongezeka

    (GMT+08:00) 2017-09-20 20:54:38

    Bei za kahawa duniani zimeongezeka kwa zaidi ya dola senti 135 kuliko bei za mwezi Juni.

    Uganda imeongeza uzalishaji ili kutumia fursa hiyo ya kuongezeka kwa bei.

    Kulingana na Shirika la Kimataifa la Kahawa (ICO) kufikia mwisho wa mwezi Agosti,bei ziliongezeka ikilinganishwa na mwezi Julai wakati ambapo bei ilikuwa senti 135 za dola ya marekani.

    Ripoti ya ICO ilionyesha kuwa katika miezi 10 ya mwanzo ya mwaka wa kahawa 2016/2017,jumala ya mauzo ya nje yalifika magunia milioni 100 ,ikiwa ni ongezeko la magunia milioni 5.7 zaidi kuliko mwaka jana wakati ambapo magunia milioni 96.3 yalisafirishwa nje.

    Ripoti hiyo ya ICO aidha inaonyesha takwimu zisizolingana za usafirishaji kahawa kutoka nchi wazalishaji.

    Nchini Brazil,mauzo ya nje katika mwezi Julai yalishuka kwa asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka jana.Kwa ujumla Brazil ilisafirisha magunia milioni 1.75 ambapo magunia milioni 1.5 yalikuwa ya kahawa ya kijani.

    Kahawa ya Arabica ilijumlisha asilimia 98.9 ya mauzo yote ya kahawa ya kijani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako