• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lionel Messi ni mto wa kuotea mbali, afunga mabao manne

    (GMT+08:00) 2017-09-21 08:23:53

    Lionel Messi alifunga mabao manne na kuwasaidia viongozi wa La Liga Barcelona kuendeleza rekodi yao ya kushinda mechi zote msimu huu kwa kuandikisha ushindi mkubwa dhidi ya Eibar.

    Messi alifunga mkwaju wa penalti na kuwaweka wenyeji hao kifua mbele kabla ya Paulinho kufunga la pili kwa kichwa. Messi alifunga mabao mawili katika muda wa dakika moja kabla ya kubadilishana pasi murua na Aleix Vidal na kufunga bao lake la nne dakika za mwisho kwenye mechi hiyo.

    Ushindi huo unawaweka Barcelona uongozini wakiwa na alama 15, alama tano mbele ya Sevilla walio wa pili ingawa Barca wamecheza bao moja zaidi.

    Mshambuliaji huyo wa Argentina amefunga mabao tisa mechi zake nne za karibuni La Liga. Bao lake la nne Jumanne limefikisha 301 idadi ya mabao ambayo amefunga Nou Camp katika kipindi cha miaka 13.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako