• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bifu zito lafukuta kati ya Neymar na Cavani wa PSG

    (GMT+08:00) 2017-09-21 08:24:19

    Bifu zito lafukuta ndani ya klabu ya matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain baina ya mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa,Neymar da Silva Santos Junior dhidi ya Edinson Roberto Cavani Gomez wote wakiwa wanakipiga katika timu hiyo.

    Chanzo cha bifu hilo la Neymar mwenye umri wa miaka 25, dhidi ya Cavani kinatokana na mchezaji huyo kunyimwa nafasi ya kupiga penati katika mchezo wa PSG dhidi ya Lyon.

    Kwa mujibu wa habari kutofautiana kwa wachezaji hao wa PSG kuliendelea hata walipoingia vyumba vya kubadilishia nguo hali iliyopelekea mchezaji, Thiago Silva kuingilia kati swala hilo.

    Kitendo cha Cavani kumsukuma Neymar kupiga adhabu ya penati ambayo PSG waliipata dhidi ya Lyon kimeonekana kama sio kitendo kizuri machoni mwa watu jambo ambalo ameonekana kuwahi kufanya hivyo hata hapo kabla.

    Kiongozi wa klabu hiyo hakufurahishwa na kitendo kilichofanywa na Cavani kiasi kwamba kuamua siku chache zijazo mchezaji sahihi atakeyeruhusiwa kupiga adhabu ya mikwaju ya penati pale itakapo tokea ndani ya kikosi cha Paris Saint-Germain.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako