• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan kutembelea kambi za wakimbizi nchini Sudan licha ya ripoti kuhusu ziara yake kupingwa

    (GMT+08:00) 2017-09-21 08:53:54

    Rais Omar al Bashir wa Sudan anatarajiwa kutembelea kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma katika jimbo la Darfur, licha ya kuwepo kwa habari za maandamano ya kupinga ziara yake, ambayo itakuwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi mwandamizi wa Sudan kwenye kambi hiyo.

    Gavana wa Jimbo la Darfur Bw Adam Al Faki amesema maandalizi yote ya ziara yake yamekamilika, na kusema kuna habari kwenye mitandao ya kijamii kuhusu watu wanaopinga ziara yake, lakini watu hao ni asilimia ndogo, sehemu kubwa ya wakimbizi hao wanakaribisha ziara yake.

    Habari zinasema watu wanaoishi kwenye kambi hiyo wameiomba tume ya umoja wa mataifa na umoja wa Afrika UNAMID, iwape ulinzi wafanya maandamano ya amani ya kupinga ziara ya Rais Omar al-Bashir.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako