• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maeneo ya kampuni za teknolojia za juu, kilimo na majaribio ya maendeleo endelevu yachangia juhudi za kuhimiza uvumbuzi nchini China

    (GMT+08:00) 2017-09-21 18:12:54

    Ripoti iliyotolewa jana na wizara ya sayansi na teknolojia ya China inaonesha kuwa, mwaka jana thamani ya uzalishaji mali wa maeneo ya kampuni za teknolojia za juu ilichukua asilimia 10 ya thamani ya uzalishaji mali wa China, na kuongoza katika kuhimiza shughuli za uvumbuzi na mageuzi ya muundo wa utoaji, wakati huohuo maeneo ya kampuni za teknolojia za kilimo yamekuwa nguvu muhimu ya kusukuma mbele maendeleo ya kilimo cha kisasa, na kupunguza tofauti kati ya miji na vijiji, huku maeneo 189 ya majaribio ya maendeleo endelevu yakisambaa kote nchini China, na kuwa na mustakabali mzuri.

    Maeneo ya kampuni za teknolojia za juu, maeneo ya teknolojia za kilimo na maeneo ya majaribio ya maendeleo endelevu ni sehemu muhimu ya kuhimiza uvumbuzi nchini China. Wizara ya sayansi na teknolojia imetoa ripoti ya mwaka 2016 kuhusu uchunguzi kwa shughuli za uvumbuzi katika maeneo muhimu nchini China, baada ya kuchunguza uwezo wa uvumbuzi wa maeneo ya kampuni za teknolojia za juu, maeneo ya teknolojia za kilimo na maeneo ya majaribio ya maendeleo endelevu, kwa kuunda mfumo wa vigezo unaojumuisha takwimu za mwaka 2014 na 2015. Ripoti hiyo imesema wakati kasi ya ongezeko la uchumi wa China imepungua na kuwa tulivu, thamani ya uzalishaji mali wa maeneo ya kampuni za teknolojia za juu yamepata ongezeko kubwa, ambalo wastani wake kati ya mwaka 2011 hadi 2015 ni asilimia 17.4 kwa mwaka. Mwaka jana, thamani ya uzalishaji mali wa maeneo 146 ya kampuni za teknolojia za juu ilichukua asilimia 11.8 ya thamani ya uzalishaji mali wa China. Naibu mkurugenzi wa idara ya maendeleo na matumizi ya teknolojia za juu iliyo chini ya wizara ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Cao Guoying amesema, maeneo ya kampuni za teknolojia za juu ni chanzo muhimu cha shughuli mpya nchini China. Anasema,

    "Kati ya kampuni 100 kubwa zaidi za mtandao wa Internet nchini China, 96 zimezaliwa katika maeneo ya kampuni za teknolojia za juu, huku 104 kati ya kampuni 131 za Unicorn zikiwa katika maeneo hayo. Hadi sasa katika maeneo hayo, kuna kampuni 404 zenye mapato ya zaidi ya yuan bilioni 10 sawa na dola za kimareani bilioni 1.5 kwa mwaka, na kampuni 10 zenye mapato ya yuan zaidi ya bilioni 100. Maeneo hayo hasa yaliyoko katika miji ya Beijing, Shanghai, Shenzhen na Zhejiang yamezaa kampuni kadhaa za teknolojia za juu zinazojulikani duniani, zikiwemo Xiaomi, Huawei na Alibaba."

    Tangu China ianze majaribio ya kujenga maeneo ya kampuni za teknolojia za kilimo mwaka 2001, imekamilisha mtandao wa maeneo hayo kote nchini China. Wizara ya sayansi na teknolojia ya China ilitathmini uwezo wa uvumbuzi wa maeneo 118 ya kampuni ya teknolojia ya kilimo nchini China. Mchunguzi wa idara inashughulikia mambo ya vijijini ya wizara hiyo Bw. Wang Zhe amesema, katika miaka ya hivi karibuni, maeneo hayo yametenga pesa nyingi zaidi kwa ajili ya shughuli za uvumbuzi, na kujenga majukwaa mengi za uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo. Anasema,

    "Eneo la kampuni ya teknolojia ya kilimo la Wuhan lilitoa mazingira ya hali ya juu kwa uzalishaji na maisha ya watu, na kukidhi mahitaji yao ya kufanya uvumbuzi, ni mfano mzuri wa kuigwa kwa maeneo mengine ya kisasa ya kampuni za teknolojia za kilimo. Eneo la Yangling limewasaidia wakulima kuongeza kipato chao kwa kutafuta mfumo wa kisasa wa kilimo, ongezeko ambalo linashika nafasi ya kwanza ikilinganishwa na sehemu nyingine mkoani Shaanxi kwa miaka 6 mfululizo."

    Maeneo ya majaribio ya maendeleo endelevu yameanza kwa kuteuliwa na idara kadhaa ikiwemo wizara ya sayansi na teknolojia ya China. Ripoti ya wizara hiyo inaonesha kuwa, kuanzia mwaka 1986 hadi mwishoni mwa mwaka 2016, China ilikuwa imejenga maeneo 189 ya aina hiyo, ambayo yako katika mikoa na miji mbalimbali nchini China. Mkurungezi wa idara ya teknolojia za maendeleo ya jamii iliyo chini ya wizara ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Wu Yuanbin amesema, maeneo hayo yameeneza mawazo ya maendeleo endelevu, na kutoa mchango muhimu katika kuhimiza uwiano wa maendeleo ya uchumi na jamii. Anasema,

    "Badala ya bajeti na sera za kipaumbele za serikali, ujenzi wa maeneo hayo unategemea matumizi na uenezaji wa teknolojia na mageuzi na uvumbuzi wa sera. Maeneo hayo pia yametafiti na kukamilisha mifumo kadhaa ya maendeleo endelevu, kama vile mfumo wa Anji, Zhejiang wa ujenzi wa vijiji vizuri, mfumo wa Gongcheng, Guangxi wa kilimo kisicholeta uchafuzi, na mfumo wa Kuqibu, Mongolia ya Ndani wa kukinga jangwa. Uzoefu na mifumo hiyo ya maendeleo endelevu, imekuwa mfano wa kuigwa katika sehemu nyingine nchini China, na hata duniani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako