• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kasi ya treni ya kati ya Beijing na Shanghai yafikia 350

    (GMT+08:00) 2017-09-21 18:23:05

    China leo imeongeza kasi ya treni za mwendo kasi katika njia ya Beijing – Shanghai na kufikia kilomita 350 kwa saa, na kuzifanya kuwa treni za kasi zaidi, miaka sita baada ya kupunguza kasi yake na kufikia kilomota 300 kwa saa.

    Ongezeko la kasi litapunguza muda wa safari kati mji wa Beijing na Shanghai yenye umbali wa karibu kilomita 1,500 na kufikia saa 4 na dakika 28. Treni hizo ni moja kati ya treni zinazofanya safari nyingi zaidi nchini China kwa kuwa inaunganisha mji mkuu wa China, Beijing ulioko kaskazini, na mji wa kibiashara wa Shanghai ulioko kusini, na kwa mwaka, treni hizo zinabeba abiria zaidi ya milioni 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako