• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yakosoa michakato ya kutayarisha bajeti ya Kenya, Uganda na Tanzania,

    (GMT+08:00) 2017-09-21 18:30:37

    Shirika la fedha la kimataifa IMF limekosoa michakato ya kutayarisha bajeti ya Kenya, Uganda naTanzania, ikiitaja kuwa isio na malengo ya baadaye na hivyo kuwa na makadirio yasioweza kufikiwa.

    IMF ilitoa wito kwa wizara za fedha kwenye nchi hizo kuajiri wataalam walio na ujuzi kwenye sekta za fedha na uchumi na pia wanaelewa utawala ili kusaidia kutayarisha bajeti zinazokidhi malengo ya muda mfupi na muda mrefu.

    Kwa sasa wakati wa kutayarisha bajeti wizara mbalimbali hutuma maombi yao kwa wizara ya fedha huku wizara hiyo ikizingatia tu maswala matatu, sera, athari za sheria mpya na mfuko wa bei.

    Lakini kwenye nchi zilizoendelea wizara za fedha huzitaka wizara zote kutoa maelezo ya kina kueleza ni kwa nini wanahitaji kiasi wanachopendekeza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako