• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shughuli ya kutangaza utalii wa Sudan yafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2017-09-21 18:54:23

    Shughuli ya kutangaza utalii wa Sudan yenye kaulimbiu ya "Sudan inayofungua mlango, Ardhi inayovutia" imefanyika katika kituo cha mawasiliano ya utamaduni na diplomasia ya umma hapa Beijing. Shughuli hiyo inalenga kutangaza rasilimali za utalii za Sudan na uwezo wa maendeleo kwa China, kujulisha juhudi zilizofanywa na serikali ya Sudan katika kuinua mazingira ya utalii na kuvutia uwekezaji kutoka nchi za nje, na kuhimiza watalii wa China kwenda nchini Sudan.

    Balozi wa Sudan nchini China Bw. Omar Issa Ahmed amesema, nchi hiyo ina rasilimali za kipekee za kitalii, hazina za utamaduni wa kale, mandhari nzuri ya kiasili na watu wakarimu, ambazo hizo ni mali halisi za Sudan..

    Mkuu wa kituo cha diplomasia ya umma cha China Bw. Ma Zhenxuan amesema, ushirkiano wa kitalii ni njia na jukwaa muhimu la kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya China na Sudan. Amesema ushirikiano huo utaendelea kuimarika, huku urafiki kati ya pande mbili ukizidi kuleta maendeleo makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako